Wednesday , 2nd Apr , 2014

Baadhi ya wanasheria ambao ni wanafunzi wa Profesa Issa Shivji wameibuka na kusema kuwa matamshi ya mwalimu wao kuhusu katiba mpya yanapingana na maandiko yake ambayo yametumika kufundishia Chuo Kikuu kwa zaidi ya miaka 30.

Mjumbe wa bunge maalum la Katiba, Ismail Jusa

Akizungumza na wandishi wa habari mjini Dodoma mjumbe wa bunge maalum la Katiba, Ismail Jusa amesema amestushwa na hatua ya Prof. Issa Shivji kupingana na muundo uliopendekezwa kwenye rasimu ya katiba ambao ulisababisha profesa huyo afanye utafiti juu ya muungano wa Tanzania na kuandika vitabu kadhaa ambavyo vimetumika kufundishia watu wengi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye pia ni mwanafunzi wa Prof. Issa Shivji amesema maswali yote aliyouliza mwalimu wake yatajibiwa kwa kutumia machapisho ya Prof. Shivji wakati wa kujadili rasimu ya Katiba ndani ya bunge maalum la Katiba katika mjadala ambao umeanza rasmi.