Thursday , 19th Nov , 2015

Mkali wa muziki Jae Baz sasa kuja na ngoma mpya ijulikanayo kwa jina la ‘your case’ siku ya jumatatu November 23 ambayo anasema ni wimbo wa mapenzi, akijaribu kuelezea hisia zake mapenzi kwa mwanamke ampendaye kwa dhati.

Akizungumzia wimbo huo, Jae Baz ameelezea wimbo huo wa ‘ your case’ kama moja ya nyimbo anazoamini zitafanya vizuri sana katika soko la muziki kwani ni wimbo alioimba kwa hisia kali sana za mapenzi

“ Najaribu kuelezea fikra zangu juu ya mwanamke ninayotamani kukutana naye na kufurahi naye pamoja na kufanya mambo mengi nayeye, hivyo naomba watu wakae tayari kuupokea wimbo huu siku ya jumatatu November 23, kupitia Television mbalimbali na pia mitandao ya kijamii”. Alisema Jae Baz

Jae Baz ni msanii anayeweza kuimba na pia ni Rapper ambaye alitamba sana na ngoma iitwayo ‘old friends’, mbali na hayo Jae Baz pia ni Director anayefanya video mbalimbali za muziki, filamu na mtangazo tofauti