
Mwana FA ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa sio lazima kufanya kitu ambacho huna uhakika nacho, hata kama kinaingiza pesa nyingi.
“Iko so obvious muziki umebadilika sana, umetoka katika ile misingi iliyowekwa na sababu zake za kuwepo, umekuwa kuhusu starehe na hela peke yake, yani ile misingi imebadilika sana, na vitu vingi ambavyo vilikuwa vinapingwa vilionekana vya kipumbavu mwanzoni huko, sasa hivi ndo kama style, yani vile vitu ambavyo vilikuwa vinapingwa ndio ambavyo watu wanafanya kwa sababu watu wanataka kutrend watengeneze hela”, alisema Mwana FA.
Pamoja na hayo Mwana FA amekiri kweli muziki wa Hip Hop sasa hivi umekuwa wa biashara, lakini amewataka wasanii kufanya kitu kingine kuliko kutumia kivuli cha muziki wa Hip Hop kuingiza pesa, kitendo ambacho kinaharibu muziki huo ambao ni muhimu kwa jamii.
“Muziki umekuwa biashara kiukweli, kama unaleta hela why not watu wachukue hela zao, lakini ninachopinga ni kuipoteza kabisa Hip Hop kwa sababu ya hela, kuna vitu vingi vya kufanya na bado ukapata mkate wako wa kila siku, sio lazima usingizie unafanya hii aina ya muziki tunayoifanya wakati huna talent hiyo, sio lazima kujisingizia kufanya kitu ambacho huna uwezo nacho ili tu uingize hela”, alisema Mwana FA.