Tuesday , 10th Nov , 2015

Vijana wametakiwa kuchangamkia fursa ya kushiriki kwenye mashindano yanayowashirikisha wajasiliamali kama njia ya kuendeleza mitaji,kusimamia na kupata taaluma ya uendeshaji wa miradi ya kimaendeleo.

Meneja wa Maswala ya Kisheria na Ushirika wa kampuni ya TOTAL Tanzania Bi. Marsha Msuya

Akizungumza jana Jijini Dar es Salaam katika shindano la ubunifu wa miradi ya Maendeleo, Meneja wa Msuala ya kisheria wa kampuni ya Total, Bi. Martha Msuya amesema wanalenga kuwawezesha vijana kutekeleza miradi bora kibiashara.

Bi. Martha amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutawawezesha vijana wajasiriamali kuzlisha bidhaa zitakazoliondolea taifa utegemezi wa bidhaa kutoka mataifa ya nje ya nchi.

Aidha ameongeza kuwa wanalenga kuibua miradi mipya kutoka kwa wananchi na kuwafundisha namna ya kuisimamia ili kufikia malengo yaliyokususiwa ikiwemo uanzishwaji wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira kwa kuchangia maendeleo.