
Mara ya mwisho Alicia Keys Alishiriki Mbio hizo mwaka 2007 na kuamua kuwa hatoshiriki tena, lakini mwaka huu kaka yake amefanikiwa kumshawishi kuungana nae katika mbio za mwaka huu.
"Nilifikiria kuwa huu ni mji wangu, sasa kwa nini isiwe!?", alisema Alicia Keys.
Pia Alicia Keys amesema sababu nyingine ya yeye kushiriki mbio hizo ni kupromote Taasisi yake aliyoianzisha ya kusaidia watoto wenye mahitaji Afrika.
"Na kizuri zaidi hii sio kwa ajili ya mimi tu, ni kuhusu kuunga mkono Keep CHild Alive, ambayo muasisi mwenzangu na mimi tuliianzisha kuokoa maisha ya watoto wanaotumia dawa za HIV, na familia ambazo hazina uwezo wa kufikia matibabu, hiki ndicho kinachovutia, mafunzo yangu ni bure ukilinganisha na wanayokutana nayo familia hizi", alisema Alicia Keys.
Mpaka sasa Alicia Keys na Taasisi wameshasadia watoto nchi Kenya, Rwanda, South Afrika, Uganda na Indiakwa msaada wa madawa, chakula na kisaikolojia.