Mwenyekiti wa kamati ya Maudhui ya Utangazaji wa TRCA Bi. Margaret Munyagi
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya Utangazaji wa TRCA Bi. Margaret Munyagi amesema kuwa lazima vyombo vyote vya habari nchini kutangaza matokeo toka kwa vyombo vyenye mamlaka ya kusimamia uchaguzi na vyanzo vya kuaminika tu na si vinginevyo.
Bi Munyagi ameongeza kuwa kwa wastani vyombo vya habari vingi vimejitahidi kuripoti maudhui mazuri japo bado kuna baadhi ya vyombo havikuzingatia mizani ya habari zao kwa kupendelea baadhi ya wagombe na kutoa habari za upande moja tu.
Kwa upande wake afisa mkuu wa utangazaji Andrew Kisaka amesema kama vyombo vya habari vikikiuka sheria za utangazaji basi wanaweza kupewa Onyo, faini hadi chombo kufungiwa kabisa na kunyang'anywa leseni.

