Friday , 16th Oct , 2015

Aliyekuwa msimamizi wa msanii wa muziki Young Dee, Maxmillian Rioba amezua mjadala mkubwa mtandaoni baada ya kuibua tuhuma nzito zinazoelekezwa kwake Young Dee kupotea kwake kimaadili, akiwa sasa na ukaribu na makundi ya marafiki wabaya.

Aliyekuwa msimamizi wa msanii wa muziki Young Dee Maxmillian Rioba

Baadhi ya maneno ya Tuhuma kutoka kwa Max yananukuliwa hapa Ya kisomeka “Kama usiposhtuka sasa hivi na kugundua kuwa huna hata chumba cha kupanga au hata begi la nguo Halafu unajiita Msanii wa muziki utastuka when it's very late. Washkaji zako wote ni wahuni, bangi, cocaine, pombe na madem wasiojua hata kuandika aeiou. Hayo sio maisha!”

Kutokana na Young Dee kukana mara kadhaa tuhuma hizo kupitia mahojiano mbalimbali tuliyowahi kufanya naye, leo hii zoezi la kumpigia simu kutafuta ufafanuzi limefanyika bila mafanikio baada ya simu yake kuwa inakatwa.

Jitihada zinaendelea kwa karibu kufuatilia sakata hili zito ili kupata mustakabathi wake.