Friday , 25th Sep , 2015

Msanii wa Bongo Flava Nuh Mziwanda amelitaka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuboresha huduma zao na kuangalia jinsi tasnia ya muziki kwa sasa inavyokwenda kwani muziki huo unafanywa na vijana.

Nuhu ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kwamba lazima BASATA wawe wanakwenda na wakati na kuboresha huduma zao.

"Wale wazee ambao wako nadhani BASATA wasidhani kuwa muziki huu ni muziki ule, sasa hivi muziki umechange, wasanii wengi ni vijana sasa hivi sio wazee tena, kikubwa zaidi ni kuboresha huduma zao, kuboresha pia vitu vyao na wao pia wawe updated kwa kila kitu ambacho kinatokea sasa hivi", alisema Nuhu.

NUhu pia amelipongeza Baraza hilo la sanaa Tanzania kwa kusema wanafanya kazi nzuri na kuwakumbusha wanachotakiwa kukifanya kwa maadili ya muafrika.

"Mi nawapa big up ni kazi nzuri wanaifanya wanakuwa wanatufanya sisi tunakuwa atention kuna msanii inakluwa kuna vitu vitu tunashindwa kuvifanya kwa maadili yetu waafrika", alisema Nuhu.