Tuesday , 22nd Sep , 2015

Watanzania wametakiwa kuchangamkia fursa zinazotolewa na benki nchini kwa vile zimeleta ukombozi mkubwa wa maendeleo ya watu na nchi.

Kauli hiyo imetolewa na waziri wa fedha wa Zanzibar Mhe. Omar Yussuf Mzee wakati akizungumza na wadau na wageni waalikwa wa benki ya NMB, mara baada ya kuzindua huduma za kadi za fedha za mastercard.

Mh. Mzee amesema benki hiyo imekuwa ni moja ya benki iliyoleta mabadilko makubwa ya serikali ya Tanzania huku ikidhihirisha kuwa serikali haikufanya makosa ilipoibinafsisha benki hiyo miaka 10 iliyopita.

Mapema Mkurugenzi wa idara ya wateja binafsi Abdulmajid Nsekela amesema kuzinduliwa kwa kadi hizo tatu kutawezesha watanzania kuendelea kibiashara na kuzidisha kasi ya maendeleo ya nchi.