Afisa Sheria wa Wizara ya Mawasiliano, Eunice Masigati akizunzungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na sheria za makosa ya mitandao
Sheria mpya ya mtandao iliyoanza kutumika Septemba mosi mwaka huu imetajwa kuleta mafanikio kutokana na baadhi ya watu wanaotumia mitandao kinyume cha sheria hiyo kutiwa hatiani.
Akizungumza kwenye kikao cha kuwajengea uwezo maofisa watekelezaji wa sheria ya makosa ya mtandao na ile ya miamala ya Kielektroniki, zote za mwaka 2015, mkuu wa kitengo cha mawasiliano serikalini, kutoka Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi. Prisca Ulomi amesema sheria hiyo imeshaanza kuonesha mafanikio.
Bi. Prisca ameongeza kuwa mpaka sasa kuna kesi ambazo zimeshafunguliwa kuhusiana na watuhumiwa wa makosa ya mitandao na wengine bado wanatafutwa kutokana na kubainika kufungua akaunti feki na kufanya udanganyifu.
Mwanasheria wa wizara hiyo Bi, Eunice Masigati amesema baadhi ya vipengele vya sheria vina mlinda moja kwa moja mtuhumiwa na kumtia hatiani hivyo wananchi wasiogope kutoa taarifa endapo wataona amechafuliwa au mtu kujipatia kipato kupitia jina lake au akaunti yake.




