Rais wa Mpira wa Kikapu mkoa wa Dar es salaam Mwenze Kabinda amesema, ligi ya Mkoa inatarajia kushirikisha timu 12 za wavulana na sita za wasichana ambapo tayari zipo kwenye maandalizi.
Mwenze amesema, uongozi kwa ujumla unaendelea na maandalizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusaka wadhamini watakaosaidia kufanikisha ligi hiyo.




