Thursday , 17th Sep , 2015

Klabu ya Yanga imesema, wanachama wanatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kuipitia katiba ambayo imeshafanyiwa marekebisho kwa ajili ya kupanga tarehe rasmi ya uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Yanga Jonas Tiboroha amesema, amesema moja ya kitu kilichochangia kutokufanyika kwa uchaguzi ni kufanya marekebisho ya katiba hivyo wanachama wanatakiwa kukutana ili kuweza kuipitia katiba yao.

Tiboroha amesema, ni lazima wanachama kukutana ili kupanga tarehe kwani uchaguzi ni haki ya wanachama kwani uongozi uliopo hivi sasa uliongezewa muda ili kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kufanya marekebisho ya katiba hiyo.