Katibu mkuu wa TSA anayemaliza muda wake Noel Kihunsi amesema, zoezi la kuchukua na kurudisha fomu za kuwania nafasi za uongozi katika chama hicho lilianza Septemba 10 na linatarajiwa kufikia tamati Septemba 30 mwaka huu.
Kihunsi amesema, awali uchaguzi huo ulitarajiwa kufanyika mkoani Morogoro lakini baadaye wadau wa mchezo huo visiwani Zanzibar waliomba kuwa wenyeji hivyo chama hakikuona sababu ya kuwakatalia.
Kihunsi amesema, kwa upande wake bado hajaamua kama atagombea nafasi nyingine katika chama hicho kwa kuwa katiba ya TSA haimruhusu kutetea tena nafasi ya ukatibu mkuu.




