Mgombea Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Juma Duni Haji
Hayo yamebainishwa na mgombea mwenza wa urais CHADEMA, chini ya UKAWA Juma Duni akiwa katika kampeni za uchaguzi katika jimbo la Lupembe mkoani Njombe ambapo wananchi waliulizwa juu wa kero walizonazo katika jimbo hilo.
Duni amesema kuwa wananchi wa Lupembe wakiwachagua UKAWA mwezi Disemba mwaka huu kiwanda hicho kitaanza kushughulikiwa na kuanza kufanya kazi na vijana wa eneo hilo kuanza kupata ajira katika kiwanda cha nyumbani huku wazazi wao kuanza kuingiza fedha kutokana na uuzaji wa chai.
Amesema wakichagua Ukawa na kuwapelekea mgombea ubunge wa Ukawa, anaye gombea kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Edwin Swale na madiwani wake alisema kuwa mbunge wao apeleke matatizo yao ya kiwanda na mendine ili yaanze kushughulikiwa na kuanza kunufaika na kiwanda hichio.
Awali wananchi walipo pewa nafasi ya kuyasema matatizo yanayo wakabili mmoja wa wananchi Magreth Kabelege amesema kuwa katika jimbo hilo wanakabiliwa na changamoto ya kufungiwa kiwanda chao ambacho walikuwa wakikitegemea kwa kuingiza kipato chao cha kila siku.
Mgombea wa Ubunge Edwin Swale amesema kuwa akipewa kura za kutosha na wananchi wa jimbo hilo atahakikisha kuwa wananchi wanapata kiwanda hicho kwa kupeleka kwa ngazi ya juu ili kishughulikiwe na kuanza kuingiza kipato chao na kufanya maisha kuwa rahisi na vijana kuwa na ajira.
Amesema kuwa wananchi wampe kura za kutosha katika ili kuweza kuingia bungeni na kutetea maslahi ya jimbo lake na huku akisema kuwa wananchi wa jimbo hilo wanatarajiwa kuingizwa katika mtego wa deni kubwa na moja ya kiwanda ambacho kinatarajiwa kuanzishwa katika maeneo yao.
Amesema kuwa wananchi hao wanatarajia kusainishwa mkataba na kiwanda cha chai ambacho wananchi watakopeshwa hisa na baadaye wataanza kudaiwa pesa nyingi ambazo zitakuwa ni mzigo.