Thursday , 27th Mar , 2014

Bodi ya ligi Tanzania TPL Board imesema kuwa suala la azimio la Bagamoyo la kuvitaka vilabu vya ligi kuu Tanzania bara kusajili wachezaji watatu wa kimataifa ni suala ambalo linazungumzika na makubaliano ya kuachana na mpango huo ni suluhisho la sok

Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Silas Mwakibinga amesema kuwa tayari baadhi ya vilabu vitaathilika na mpango huo na pia maoni ya wadau wengi yanaonyesha wazi kuwa mpango huo hauna manufaa kwa soka la kisasa

Aidha Mwakibinga amesema kuwa wadau wengi wanaamini uwepo wa wachezaji wa kigeni wenye sifa na ubora ni faida kwa taifa kwani wataleta ushindani kwa wachezaji wetu na wataongeza ujuzi na mbinu mpya kwa wachezaji wetu badala ya kukaa na kutumia wachezaji wa nyumbani pekee kitu ambacho hakitakua na faida katika soka hili la utandawazi.