Frasha
Frasha ameeleza kuwa, yeyote anayempinga gavana huyo Dk. Alfred Mutua na mkakati wake unaotambulika kama maendeleo 'Chapchap', ni adui wa maendeleo, akisisitiza kuwa katika wakati huu wa changamoto kwake yupo pamoja naye.
Mbali na hilo kwa sasa Frasha ambaye pia amejikita kuendesha project pembeni ya kundi, anafanya vizuri katika chati kupitia kolabo aliyofanya na Timmy Tdat na Mchizi Gaza, kazi ambayo unaitazama sasa kupitia eNewz ikiwa inasimama kwa jina “Shigidi”.

