Wednesday , 2nd Sep , 2015

Kikosi cha wachezaji 23 cha Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kimeingia kambini leo kujiandaa na mechi ya kuwania kufuzu fainali za AFCON dhidi ya Nigeria itakayochezwa Jumamosi hii uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Baraka Kizuguto amesema, timu iliwasili ikiwa na wachezaji 21 ambapo mchezaji Abdi Banda hakuweza kuingia kambini kutokana na majeruhi na wachezaji 20 walioingia kambini walijumuika na wachezaji watatu ambao ni Mrisho Ngassa anayeichezea timu ya Fre State ya Africa Kusini, Mbwana Samatta na Thimas Ulimwengu wote wa TP Mazembe ya nchini DRC Congo.

Kizuguto amesema, Stars inaendelea na mazoezi leo jioni Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo hapo kesho kitaendelea na mazoezi huku siku ya Ijumaa wachezaji wa Stars wakifanya mazoezi mepesi kwa ajili ya kuwasubiri wapinzani Super Eagles ya Nigeria ambao watawasili nchini kesho au Ijumaa.