Awali Taifa Stars ilikuwa ipitie Muscat nchini Oman kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo, lakini kutokana na shirikisho la soka la Oman kushindwa kukidhi mahitaji ya kanuni za FIFA za uandaaji wa mechi ya kimataifa ya kirafiki sasa mchezo huo hautakuwepo tena.
Stars inatarajiwa kuondoka Jumapili usiku na kuwasili Istanbul siku ya Jumatatu majira ya saa 5 kamili asubuhi, kisha kuelekea Kocael ambapo ndio itakua kambi yake ya wiki moja.

