
Kufuatia uamuzi huo Waziri Nyalandu amemtangaza Bi. Devotha Mdachi kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania wakati mchakato wa kumpata mkurugenzi mpya ukiendelea.
Aidha, Waziri Nyalandu ameiagiza Bodi ya Utalii kuitangaza nafasi hiyo kwa Watanzania wenye sifa kote duniani, ili waombe kazi hiyo ndani ya siku 21 kuanzia kesho Machi 25. Amesema pia kwamba Dkt. Aloyce Nzuki atapangiwa kazi nyingine.