Saturday , 25th Jul , 2015

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira wilaya ya Iringa mjini (IRUWASA) inatarajia kuongeza gharama ya ulipiaji wa hudumu hiyo kwa wateja wake ili kuboresha utoaji wa huduma zake.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amesema kutokana na wananchi kutolipia huduma hiyo kikamilifu na kwa wakati imepelekea IRUWASA kushindwa kuboresha utoaji wa huduma hiyo.

Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira inatarajia kuongeza gharama ya malipo ya huduma ya maji kutoka shilingi 980 hadi 2000 kwa uniti moja ambapo wananchi wamesema ongezeka hilo litapelekea kuongezeka kwa ghalama za maisha.

Kwa upande mkurugenzi mtendaji wa IRUWASA mkoa wa Iringa Bw. Marko Mfugale amesema ongezeko la gharama hizo imetokana na kuongezeka kwa bidhaa kama dawa za kutibia maji na ulipiji wa nishati ya umeme.

Hata hivyo; IRUWASA inashirikiana na mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati za maji EWURA huku ikiendelea kupokea maoni ya wananchi, baraza la watumiaji wa huhuma hiyo pamoja na baraza la ushauri la serilkali ili kufikia muafaka wa kupandishwa kwa ghalama hizo.