Wednesday , 22nd Jul , 2015

Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Allan Wetende Wanga amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Azam FC, akitokea El Merreikh ya Sudan.

Usajili wa Wanga, unakamilisha idadi ya wachezaji saba wa kigeni wa Azam FC kwa mujibu wa kanuni za ligi kuu ya Soka Tanzania Bara.

Wachezaji wa kimataifa waliosajiliwa mpaka sasa katika klabu hiyo ni Jean Baptiste Mugiraneza ‘Migi’ kutoka APR ya Rwanda na Serge Wawa Pascal, Kipre Michael Balou, Kipre Tchetche wote wa Ivory Coast, Brian Majwega wa Uganda na Didier Kavumbangu wa Burundi, ambao wote waliokuwepo tangu msimu uliopita.

Awali, kulikuwa kuna mvutano baina ya pande hizo mbili, mchezaji akitaka kusaini miezi sita na klabu ikitaka angalau asaini mwaka mmoja lakini mwisho makubaliano yamefikiwa