
msanii wa muziki wa nchini Kenya Victoria Kimani
Baadhi yao wameelezea kuwa, msanii huyo amekuwa si mzalendo na mwenye uwezo mdogo, akibebwa na sapoti ya usimamizi mzuri wa muziki wake.
Majadiliano hayo yamezuka baada ya mwanadada huyo kutoa lawama zake kuwa wakenya wamekuwa na uzalendo mdogo katika kuwasapoti wasanii wao kuweza kufanya vizuri nje ya nchi, binafsi akionekana kuwa mbali na nchi yake, akiwa anasimamiwa na lebo kutoka Nigeria.
Hata hivyo, staa huyo hajaonesha kurudishwa nyuma na matani mengi ya mashabiki kuhusu muziki wake huo, na kuwashukuru wote walioshiriki kutoa maoni yao kuhusu yeye wakitumia trend ya #someonetellVictoriakimani.
