Tuesday , 7th Jul , 2015

Chama cha Demekrasia na Maendeleo (CHADEMA) leo kimeitisha mkutano wa kamati kuu huku vyama vingine vinavyounda umoja wa UKAWA navyo vikiwa vimeitisha mikutano ya vyama vyao ili kujadili matukio ya hivi karibuni yaliyotokea Bungeni.

Mwenyekiti wa CHADEMA, na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. Freeman Mbowe.

Akizungumza jana Mjini Dodoma Mwenyekiti wa CHADEMA, na Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA, Mh. Freeman Mbowe amesema kuwa ajenda kuu ya mkutano hatua ya wabunge wa Umoja wao kufukuzwa Bungeni pamoja na Miswada ya Mafuta na gesi kupitishwa.

Aidha Mh .Mbowe ameongeza kuwa kesho Jumatano watakuwa na mkutano wa pamoja kati ya wabunge na viongozi wa ukawa kujadili masula yaliyotokea Bungeni.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo mkoa wa Njombe kimesema hakikubaliani na hatua iliyo yanywa na bunge ya kuwafukuza bungeni Wabunge wa kambi ya Upinzani na wanao unda ukawa kwa kupinga hati ya dharula katika sera ya gesi na mafuta.

CHADEMA NJOMBE WAUNGA NA MAKAO MAKUU

Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kutangaza nia ya kuwania jimbo la Njombe kusini linaloshikiliwa na Spika wa bunge la Tanzania, mbunge Anna Makinda, Emmanuel Filangali, mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Njombe Faki Lulandala amesema kuwa Chadema haikubaliani na kitendo hicho kwa kuwa sera hiyo ina maslahi makubwa kwa wananchi hivyo haipaswi kupelekwa haraka.

Lulandala ambaye pia anatangaza nia ya kuwania jimbo la Njombe kusini amesema kuwa anashangaa kuona suala hilo mihumu kwa uchumi wa Watanzania kupelekwa bungeni kwa hati ya dharula wakati suala hilo likitengenezwa kwa utulivu kwa kuzipitia vipengele vilivyomo katika sera linaweza kubadilisha kilimo, na kuboresha mishahara ya watumishi.

Aidha Emmanuel Filangali amesema kuwa akipitishwa na chama chake na kuwa mbunge atahakikisha uchumi wa mkoa wanjombe unakuwa kwa kusimania pesa zinazoletwa kwaajili ya mfuko wa jimbo.

Amesema kuwa atasimamia Maendeleo vijijini na kuhakikisha vijana wa vijijini hawakimbilii mjini na kuhakikisha makusanyiko wa watu vijijini unakuwa kama zamani kwa kuhakikisha mazingira yanawawezesha vijana kujiajili huko.

Amesema kuwa anatamani Chadema kuchukua jimbo hilo lakini nafsi yake inatamani yeye kuwa mwakilishi wa wakazi wa jimbo hilo bungeni.