Monday , 15th Jun , 2015

Star wa michano wa nchini Kenya, Jua Cali ameendelea kuwafikia watoto wa mitaani kutoka sehemu mbalimbali nchini Kenya, na kuwapatia mavazi kupitia kampeni yake ya Hisani ya Ng'arisha Initiative ambayo ameianzisha hivi karibuni.

Kwa sehemu matunda ya mkakati huu yameanza kuonekana, ambapo msanii huyu kwa kushirikiana na wasamaria wema kutoka sehemu mbalimbali wameweza kukusanya nguo na kusambaza sehemu kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu huko nchini Kenya.

Jua Cali pia kupitia njia ya mtandao ameonyesha kwa sehemu matunda ya mkakati huo katika kusaidia wenye uhitaji.