Akizungumza jijini Mwanza leo wakati wa uzinduzi wa umoja wa michezo wa shule za sekondari (UMISETA) na shule za msingi (UMITASHUMTA), amesema serikali imefanikisha kuwaondoa wanafunzi kukaa mavumbini hadi katika madawati kwa asilimia 65, huku 35 iliyobaki ikitarajiwa kumalizwa baadaye.
Amesema lengo la serikali ni kutaka kuboresha elimu nchini na kuhakikisha kila shule inakuwa na madawati tofauti na miaka ya nyuma.
Aidha, amezitaka halmashauri nchini kuhakikisha kila mwaka zinatenga pesa kwa ajili ya kununulia madawati ili wanafunzi waweze kuondokana na kukaa chini ya matofauri ama sakafuni.
Pia amesema katika suala la ujenzi wa maabara, lazima ziwe zimekamilika kabla ya Juni 30 mwaka huu kama agizo la Rais Jakaya Kikwete linavyosema.
Amesema kila halmashauri inatakiwa kuhakikisha shule zote zinamaliza ujenzi wa maabara tatu kabla ya Juni 30 mwaka huu, ili ziweze kufanya kazi kuanzia julai, mwaka huu.
Aidha, pinda amesema serikali inaendelea kuhakikisha inaleta uwiano wa masomo kwa wanafunzi hususani ya vitabu kutoka kitabu kimoja kwa wanafunzi saba hadi kufikia wanafunzi watatu hivi sasa.
Na ameziagiza halmashauri za wilaya zote kuhakikisha zinapima maeneo ya shule pamoja na viwanja vyake ili kuepukana na migogoro ya ardhi inayotokea mara kwa mara.