Monday , 8th Jun , 2015

Kazi mpya kutoka kwa msanii Jaguar wa nchini Kenya, imeonesha kuendelea kumvuta msanii huyo katika siasa akienda sambamba na muziki wake, akiwa mbioni kukamilisha projekti mpya kabisa inayokwenda kwa jina Barua kwa Raisi.

msanii wa muziki Jaguar akisalimiana na Rais Kenyatta

Kupitia kazi hiyo, Jaguar ambaye ni moja ya mastaa walio karibu kabisa na uongozi wa nchi hiyo ameamua kukusanya baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo wakenya wa kawaida, na kuigiza baadhi ya mazingira magumu kuonyesha uhalisia kupitia video ya kazi hiyo itakayotoka karibuni.

Hatua hii inazidi kumsogeza zaidi star huyo katika nafasi za uwakilishi na uongozi wa wananchi hasa kutokana na moyo wake wa kusaidia wenye uhitaji, ingawa mpaka sasa hajaweka wazi endapo ana nia ya kuwania nafasi yoyote ya uongozi wa kisiasa wa nchi hiyo.