Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa ZTTA, Nassir Abdallah amesema mashindano hayo yanayotarajia kushirikisha vilabu 10 yatafanyika kwa siku tatu ambapo baada ya mashindano hayo, vilabu hivyo vinatarajiwa kushiriki mashindano ya taifa yanayotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu jijini Dar es salaam.
Abdallah amesema, baada ya kukamilika kwa mashindano ya muungano, kamati ya ufundi ya Zanzibar, itatoa ushauri wa nini kifanyike baada ya kugundua mapungufu ili Zanzibar iweze kutoa wachezaji wengi watakaounda timu ya Taifa itakayochaguliwa kwenda Congo Brazaville