Saturday , 28th Nov , 2015

Chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) kimethibitisha kuwa mwenyeji wa mashindano makubwa ya vilabu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati KAGAME CUP yanayotarajiwa kufanyika mwezi wa Julai mwakani.

Mkurugenzi wa ufundi wa ZFA Massoud Attai amethibitisha kuwa Zanzibar watakuwa wenyeji kuandaa mashindano hayo ambapo walipeleka maombi yao kwa CECAFA kwa kutaka kuwa wenyeji na CECAFA wamekubali Zanzibar kuandaa michuano hiyo.

Amesema kwa sasa maandalizi yameshaanza na tayari baraza la michezo tayari limeshapokea barua ya kuwa Zanzibar ni wenyeji wa michuano hiyo.

Katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika ndani ya visiwa vya Zanzibar timu za Mafunzo na JKU ndiyo bingwa na makamu bingwa wa ligi kuu ya Zanzibar msimu wa 2014-2015 na ndizo zitakazoiwakilisha Zanzibar.

Hii si mara ya kwanza kwa Zanzibar kuwa mwenyeji wa michuano hiyo kwani waliwahi kuwa wenyeji katika miaka ya nyuma ikiwemo mwaka 1985 na 1990.