Tuesday , 3rd Feb , 2015

Michuano ya ligi kuu Soka Tanzania Bara inaendelea kesho kwa Coastal Union kuwakaribisha Yanga Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Afisa habari wa Yanga, Jerry Muro amesema wameifuata Coastal Union wakiwa na dhamira ya kupata ushindi na kupata pointi tatu muhimu ambapo mpaka sasa wana pointi 19 baada ya kutoa sare na Ndanda FC ya Mjini Mtwara mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Kwa upande wa Coastal Union inaingia huku ikiwa na Pointi 17 kutokana na kupata sare ya bila kufungana katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.