Hayo yameelezwa na taarifa zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa jioni ya leo Mei 07, 2018 na kusema sababu kubwa ya wao siku ya jana Mei 06, 2018 kuonekana wakiwa uwanjani na jezi zisizo kuwa na 'logo' ni kutokana na kuzuiliwa na waratibu wa mashindano hayo kwasababu ya kutokuwepo kwa maelekezo ya matumizi ya wadhamini.
"Hivi sasa uongozi wa Yanga na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa pamoja tunashughulikia suala hili ili mechi zijazo nembo ya mdhamini wetu iweze kutumika kama ilivyotumika kwenye michezo ya hatua za awali. Ikumbukwe kwamba kuanzia hatua hii ya makundi, CAF ndiyo inasimamia haki za matangazo pamoja na mabango yote yanayotakiwa kuwekwa viwanjani, hivyo tayari mawasiliano nao kupitia TFF yamekwishafanyika", amesema Mkwasa.
Pamoja na hayo, Mkwasa ameendelea kwa kusema "uongozi wa Yanga unaomba radhi kwa kampuni ya SPORTPESA na wale wote walioathirika na matatizo yote yaliyojitokeza wakati wa mchezo huo".
Kwa habari kamili soma hapa chini