Friday , 18th Dec , 2015

Uongozi wa vinara wa ligi kuu ya soka Tanzania bara klabu ya Yanga, umetangaza kumsimamisha Haruna Niyonzima kwa muda usiojulikana.

Kiungo machachari wa Yanga Haruna Niyonzima akionyesha cheche zake katika moja ya mechi dhidi ya Azam msimu uliopita.

Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha amesema Niyonzima amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Tibaroha amesema Niyonzima amekuwa akifanya mambo ambayo yanaonyesha wazi ni ukiukaji wa mkataba hasa katika masuala ya utendaji ambapo amekuwa akichelewa kuwasili kambini.

Ameongeza kuwa kiungo huyo alikuwa kwenye majukumy ya kitaifa akiichezea timu yake ya taifa ya Rwanda iliyokuwa kwenye michuano ya Chalenji nchini Ethiopia lakini tangu kumalizika kwa michuano hiyo simu zake zote zilikua hazipatikani

katika hatua nyingine Tibaroha amesema wamechukua hatua hiyo ili pia iwe fundisho kwa wachezaji wengine .

Yanga ipo jijini Dar es salaam ikifanya maandalizi ya mwisho kuelekea mechi yao ya kesho watakayoumana na Stand united ya shinyanga kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ikiwa ni muendelezo wa ligi kuu ya soka ya Tanzania bara.