Tuesday , 10th Feb , 2015

Timu ya Yanga imeanza mazoezi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya BDF ya Nchini Botswana inayotarajiwa kuchezwa Ferbuari 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Afisa Habari wa Klabu hiyo, Jerry Muro amesema, timu hiyo iliyo chini ya Kocha wake Hans Van Der Pluijm inafanya mazoezi kuhakikisha kikosi kinaimarika katika nafasi ya Ushambuliaji, Kiungo na Ulinzi ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

Muro amesema, katika kikosi hicho kulikuwa na majeruhi ambao ni Mlinda Mlango Deogratius Munish Dida aliyekuwa akiugua Maralia, Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite