Friday , 17th Apr , 2015

Yanga kesho inashuka dimbani kutupa karata yao kwa Etoile du Sahel ya Tunisia, uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam katika michuano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) hatua ya 16 bora.

Akizungumza na East Africa Radio, nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub Canavaro amesema, kila mchezaji katika timu hiyo ana hamu ya kucheza mechi hiyo na wana furaha kukutana na Etoile na wanaamini watashinda kutokana na mazoezi.

Young Africans imeingia katika hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya kuzitoa BDF XI ya Botswana katika hatua ya awali kwa jumla ya mabao (3-2), kisha kuwaondoa FC Platinum ya Zimbabwe katika hatua ya kwanza kwa jumla ya mabao (5-2).

Endapo timu ya Young Africans itafanikiwa kuwaondoa Etoile du Sahel itasuburia kucheza mechi ya mtoano (Play-off) dhidi ya timu mojawapo zitakaotolewa katika 16 bora ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika (CL).