Thursday , 20th Aug , 2015

Vijana wawili anatarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Singapore kushiriki mashindano ya tano ya Dunia ya Vijana ya kuogelea yanayotarajiwa kuanza Agosti 25 mpaka 30 mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania TSA Noel kihunsi amesema, wachezaji hao ambao ni Adil Barma na Amal Gadial wataondoka hapo kesho ambapo watawasili Agosti 22 kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo inayoshirikisha vijana wenye umri chini ya miaka 18.

Kihunsi amesema wana amini waogeleaji hao watafanya vizuri kutokana na maandalizi waliyoyafanya tangia hapo awali ili kuweza kuitangaza nchi vizuri kupitia mchezo huo.