Friday , 21st Aug , 2015

Watanzania wanne wanatarajiwa kutupa karata yao hapo kesho Beijing nchini China katika mashindano ya dunia ya riadha yanayoshirikisha nchi mbalimbali duniani.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake, Fabian Joseph ambaye ni nahodha amesema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano hayo na wanaamini watafanya vizuri katika mashindano hayo.

Fabian amesema, kwa wapinzani wao wakubwa ni Kenya, Uganda na Ethiopia pia wamejiandaa lakini imani yao wameelekeza katika ushindi.

Washiriki watakaotupa karata yao hapo kesho ni Fabian Joseph, Ezekiel Gimba, Alphonce Felix watakaoshiriki mbio za marathoni pamoja na Ismail Juma atakayeshiriki mbio za mita 10,000.