Thursday , 6th Aug , 2015

Kikosi cha wachezaji 29 wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kinatarajiw akuingia kambini Agosti 9 mwaka huu kwa ajili ya kambi kujiandaa na mechi dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu AFCON.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kocha wa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema, katika kikosi hicho amewajumuisha wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi ambao baadae watajumuika kwa kambi ya kujiandaa kucheza na Nigeria Septemba mwaka huu nchini Uturuki.

Mkwasa amesema, Stars inatarajiwa kuweka kambi ya siku kumi jijini Istambul ambapo itacheza michezo miwili ya kirafiki na timu za Taifa za Libya na Kuwait kabla ya kurejea nchini kuwavaa Nigeria.

Mkwasa amesema, wachezaji watakaongia kambini jumapili ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga SC) na Aishi Manula (Azam FC), walinzi wa pembeni: Shomari Kapombe (Azam FC), Michael Aidan (Ruvu Shooting), Juma Abdul, Mwinyi Haji (Yanga SC) na Abdi Banda (Simba SC).

Walinzi wa kati; Hassan Isihaka (Simba SC), Nadir Haroub, Kelvin Yondani (Yanga SC), Viungo wakabaji: Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya (Azam FC), Viungo washambuliaji ni Salum Telela (Yanga SC) na Said Ndemla (Simba SC).

Washambuliaji wa pembeni; Orgenes Mollel (Aspire – Senegal), Abdrahman Mbambi (Mafunzo), Deus Kaseke, Saimon Msuva (Yanga SC), Ramdhani Singano, Farid Musa (Azam FC), huku washambuliaji wa kati wakiwa ni John Bocco, Ame Ally (Azam FC) na Rashid Mandawa (Mwadui FC).

Wachezaji wa kimataifa waliojumuishwa katika kikosi hicho ambacho Agosti 23 kitaelekea kambini nchini Uturuki kwa kambi ya siku kumi ni Mbwana Samata, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe – DR Congo), Mrisho Ngasa (Free State - Afrika Kusini) na Hassan Sembi (Santos FC – Afrika Kusini) na Adi Yussuf (Mansfield Town – Uingereza).