Tuesday , 28th Jun , 2016

Wachezaji watatu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya kuogelea wanaotarajiwa kushiriki mashindano ya Olimpiki wameendelea na kambi katika nchi tofauti.

Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania TSA Ramadhan Namkoveka amesema, wachezaji hao ambao ni Hilary Hilary ambaye yupo nchini Dubai na Magdalena Moshi ambaye yupo nchini Australia pamoja na Amary Gadialy ambaye wamemuongeza kwa ajili ya kuangalia mchezaji atakayefaa kuelekea katika mashindano ya Olimpiki wameendelea na kambi ambapo majina yao tayari yamepekewa chama cha kuogelea Duniani FINA.

Namkoveka amesema, wanaendelea kuangalia suala la kambi ya pamoja kama wataweza kuweka hapa Tanzania au nchi nyingine kwani licha ya Tanzania kuwa na uwezekano wa kuwekwa kambi lakini bado kunachangamoto ya kuwa na bwana la mita 50 na pia pesa ya maandalizi mpaka sasa bado hawajapata.

Namkoveka amesema, wamepata nafasi ya upendeleo ambao unataratibu zake na unaweza kuchagua mchezaji lakini FINA wakamkataa na kuhitaji mchezaji mwingine kwa kuangalia vigezo vyake.

Namkoveka amesema, nafasi ambayo wameipata inamadhumuni yake ambayo FINA wanahitaji mchezaji aliyebora zaidi ili aweze kuendeleza mchezo wa kuogelea hapa nchini.