Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC Filbert Bayi amesema, wanariadha hao wataungana na wenzao watatu ambao walikuwa katika kambi maalumu ya Eldoret nchini Kenya.
Bayi amesema wanariadha Said Makula na Alphonce Alex wanaungana na Fabian Joseph, Fabian Nelson na Basil John ambao walikuwa Kenya.
Bayi amesema, Tanzania inatarajia kuwakilishwa na wakimbiaji watatu lakini wameamua kuwaweka kwenye kambi zaidi ya watatu ambapo wengine bado hawajafuzu ili kuwapa nafasi ya kujinoa na hatimaye kuweza kupata vigezo vya kufuzu katika michezo hiyo itakayofanyika Brazili mwaka huu.
Bayi amesema, TOC inahakikisha wanariadha hao wanapata nafasi ya kushiriki katika michezo hiyo na kuweza kuleta medali.







