Akizungumza jijini Dar es salaam, Kocha wa Timu hiyo, Francis Felix amesema, wanaamini mazoezi waliyoyafanya yatawasaidia kwani washiriki wote wapo tayari kwa mashindano na wanaamini wataweza kufanya vizuri na kuitangaza nchi zaidi katika michezo hiyo.
Alex amesema,amekaa kambi ya wiki tatu kwa ajili ya kuwapa mafunzo vijana hao akiamini mashindano hayo yatakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila nchi shiriki za mashindano hayo kuhitaji ushindi.
Kwa upande wake, mshiriki wa mbio hizo, Alphonce Alex amesema, wana matumaini ya kufanya vizuri na kwenye mashindano mchezaji yeyote anatakiwa awe amejiandaa kimwili na kiakili kupambana na changamoto atakazokutana nazo ili aweze kushinda.
Timu hiyo inatarajia kuondoka kesho ikiwa na msafara wa wachezaji watano na kocha mmoja ambapo mashindanio hayo ya mbio za nyika za Dunia yataanza kutimua vumbi Machi 28.
Wanariadha hao kutoka Tanzania watakaoshiriki mbio hizo ni Joseph Panga, Fabian Nelson, Ismail Juma, Basili John na Alphonce Felix wakiambatana na Kocha Francis John.