Wednesday , 2nd Jul , 2014

Zaidi ya wanamichezo 250 kutoka Tanzania Bara na Visiwani watashiriki mashindano ya wazi ya mchezo wa kuogelea yanayotarajiwa kufanyika Septemba 26 mpaka 28 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Waogeleaji8 katika Mashindano

Zaidi ya wanamichezo 250 kutoka Tanzania Bara na Visiwani watashiriki mashindano ya wazi ya mchezo wa kuogelea yanayotarajiwa kufanyika Septemba 26 mpaka 28 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi wa chama cha Kuogelea nchini (TSA) Marcelino Ngalioma amesema kutakuwa na idadi hiyo kubwa ya wanamichezo wa kuogelea tofauti na miaka iliyopita kutokana na wananchi kupata mafunzo ya kutosha na pia kuwa na uelewa juu ya mchezo huo.

Ngalioma amesema mashindano hayo ambayo yatashirikisha washiriki kuanzia miaka nane na kuendelea yamekuwa yakifanyika katika mazingira magumu kutokana na Chama kutokuwa na eneo maalumu la kufanyia mashindano mbalimbali ya kuogelea na hivyo kupelekea kutafuta maeneo ambayo yatasaidia kuanzia mazoezi hadi mashindano yatakapowadia.