Uongozi wa klabu ya soka ya simba ya jijini Dar es salaam umewataka wanachama wake wote wanaotaraji kuwania uongozi ndani ya klabu hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao kufuata taratibu na sheria za uchaguzi wa klabu hiyo
Katibu mkuu wa klabu hiyo Ezekiel Kamwaga amesema hayo hii leo baada ya kuwepo kwa taarifa za kuanza kwa kampeni mapema kwa baadhi ya wanachama ambao wanataka kuwania uongozi kitu ambacho amesema ni kunyume na taratibu
Kamwaga ameongeza kuwa muda wa kampeni bado haujatangazwa na kamati ya uchaguzi na hivyo kwa mwanachama yeyote anayeitakia mema timu hiyo vema akatoa taarifa klabuni kama ana uthibitisho wa mtu anayevunja utaratibu huo.
