Friday , 16th May , 2014

Baada ya kuwepo kwa malalamiko kwa muda mrefu hatimaye Shirika la Kumbukumbu la taifa linataraji kuanza mkakati wa kukusanya vielelezo vya wanamichezo wa zamani wa Tanzania waliofanya makubwa ili kuweka kumbukumbu zao katika jumba la makumbusho.

Shirika la makumbusho ya taifa linataraji kuandaa maonesho maalumu ya sanaa na utamaduni ambayo yatashirikisha walemavu wa aina zote ambao watashiriki maonesho hayo yatakaoshirikisha pia wageni kutoka nchini India.

Mhifadhi historia na sanaa bi Flower Manase amesema mikakati hiyo ni katika kutekeleza maagizo ya Rais Jakaya Kikwete ambapo hivi sasa wako katika mpango mkakati wa kuanza kufungua maonesho kwaajili ya wanamichezo mbalimbali waliotukuka.

Aidha Manase amesema utaratibu wa kukusanya taarifa muhimu juu ya wanamichezo hao zinaendelea kwa kushirikiana na vyama husika vya mchezaji ambaye anastahili heshima hiyo na kinachofanyika sasa ni utafiti wa kina juu ya wachezaji hao ili kupata taarifa sahihi.