Tuesday , 21st Jun , 2016

Waamuzi kutoka nchi ya Ethiopia wanatarajiwa kuchezesha mchezo wa awali wa kuwania kushiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana Juni 25 mwaka huu kati ya timu ya Taifa ya taifa ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys dhidi ya Shelisheli.

Afisa habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kamishna wa mchezo huo atawasii nchini akitokea Malawi.

Kwa upande wake Kocha wa Serengeti Boys Bakary Shime amesema, amekiandaa kikosi chake kwa ajili ya kushidna mchezo huo ambao anaamini utakuwa na ushindani mkubwa kutokana na kila timu kuhitaji ushindi ili kuweza kusonga mbele.

Shime amewataka mashabiki kujitokeza kuipa sapoti timu yao kwani licha ya kikosi kujiandaa kushinda lakini wao kama mashabiki wanauwezo wa kuisaidia timu pia kuweza kufanya vizuri.

Kikosi cha Serengeti Boys kiliingia kambini Juni 14 mwaka huu kikiwa na wachezaji 24 wakitokea mapumziko mara baada ya kumaliza mashindano nchini India.