Sergio Aguero na Pierre-Emerick Aubameyang wakiwa na Drake katika picha tofauti
Taarifa hiyo iliyotolewa katika ukurasa wa Twitter wa klabu hiyo, haikuwa na maelezo yoyote juu ya sababu ya kusitishwa kwa hatua hiyo.
All Roma players banned from taking photos with Drake until the end of the season
— AS Roma English (@ASRomaEN) April 15, 2019
Baadhi ya wadadisi wameelezea kuwa matukio hayo ya karibuni ya wachezaji mbalimbali kupiga picha na msanii huyo yamepelekea kupoteza michezo yao.
Mtandao wa michezo wa 90min umeonesha matukio ya picha za wachezaji maarufu ambao baada ya kupiga picha na Drake, walipoteza mechi yao moja iliyofuata.
Picture with Sancho = Dortmund lose 5-0
Picture with Aubameyang = Arsenal lose 1-0
Picture with Aguero = Man City lose 1-0 and Aguero misses a penalty.
The Drake curse continues! pic.twitter.com/5dV2nkbrti
— 90min (@90min_Football) April 10, 2019
Kiungo wa Borussia Dortmund, Jodan Sancho alipopiga picha na Drake timu yake ilipoteza mchezo uliofuata kwa kufungwa mabao 5-0 dhidi ya Bayern Munich, pia mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang baada ya picha yake na Drake, timu yake ilifungwa na Everton bao 1-0 huku Manchester City ikifungwa bao 1-0 na Spurs baada ya Sergio Aguero kupiga picha na msanii huyo.