
Moja kati ya mechi iliyowahusiasha viongozi wa dini na wabunge
Katibu wa kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini Mkoa wa Dar es salaam John Solomon amesema, lengo kuu la mchezo huo ni kuhamasisha amani ya nchi na anaamini Bunge lililoanza hapo jana halitakuwa na vurugu.
Pia amesema kuwa anaamini wabunge wawapo bungeni watatofautiana kwa itikadi na hoja lakini katika mechi hiyo watakuwa pamoja na kwamba mwisho wa siku wabunge wote watakubaliana kwa manufaa ya watanzania na nchi kwa ujumla.
Solomon amesema, wanaamini mchezo huo utawaunganisha wabunge wa vyama vyote nchini na kuwafanya kuwa wamoja ili kuweka imani kwa wananchi wao.