Monday , 5th Oct , 2015

Waamuzi watakao chezesha mchezo wa kufuzu kombe la Dunia kati ya Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na Malawi (The Flames) wametajwa hii leo,ambapo wantokea Somalia.

Waamuzi watakao chezesha mchezo wa kufuzu kombe la dunia kati ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars na Malawi (The Flames) wametajwa kutokea nchini Somalia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam afisa habari wa shirikisho la soka nchini Tanzania Baraka Kizuguto amewataja waamuzi hao kuwa ni Hagi Yabarow Wiish ambaye ni mwamuzi wa kati, akisaidiwa na Hamza Hagi Abdi na Salah Omar Abubakar , huku mwamuzi wa akiba ni Bashir Olad Arab.

Aidha, Kizuguto amewataja mtathimini wa waamuzi Sam Essam Islam akitokea Misri na kamisaa wa mchezo ni Muzambi Gladmore kutoka Zimbabwe.

Pia Kizuguto ametaja viingilio vya mchezo huo ni cha juu kabisa kwa mchezo huo shilingi elfu kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani ikiwa ni shilingi elfu tano (5,000).

Wakati huo huo timu ya taifa ya Malawi (The Flames) imewasili nchini jana saa 4 asubuhi na kufikia katika hoteli ya De Mag iliyopo Mwanayamala, ambapo kikosi hicho leo kimefanya mazoezi asubuhi katika uwanja wa Boko Veterani na kesho kitafanya mazoezi kwenye uwanja wa Taifa.

Wachezaji wa kimataifa wa Tanzania Mrisho Ngassa amewasili kambini tangu jana akitokea Afrika Kusini, huku Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu nao wakiwasili kutoka DRC Congo.