Saturday , 24th May , 2014

Ushauri umetolewa kwa wakuu wa vyuo vikuu hapa nchini kuhamasisha michezo mbalimbali katika vyuo vyao na kuhakikisha wanapata timu bora za kushiriki michuano mbalimbali ya ndani na nje

Pichani ni moja ya wanamichezo toka chuo cha mtakatifu Paul waliposhiriki michuano ya vyuo vikuu EA iliyofanyika mwaka jana nchini Tanzania

Makamu wa Rais wa shirikisho la michezo kwa vyuo vikuu vya Afrika Mashariki FEAUG Noel Kihunsi amesema atatumia nafasi yake kuvihamasisha vyuo vya Tanzania kuhakikisha vinajiandaa na kushiriki michuano ya msimu huu itakayofanyika nchini Uganga mwezi Desemba mwaka huu.

Kihunsi amesema alishangazwa sana kuona mashindano yaliyopita ambayo Tanzania ilikua mwenyeji ikishuhudiwa vyuo 8 pekee kati ya 25 vikishiriki michuano hiyo kitu ambacho kilipelekea kukosekana kwa ushindani wa kutosha katika michezo mbalimbali ambayo vyuo vyetu vimekuwa vimeshiriki

Kihunsi amesema kujitokeza kwa idadi kubwa ya vyuo vitakavyokua vikishiriki kwa wingi kunapanua nafasi ya kushinda katika michuano mbalimbali ndio maana ameona ni bora kuhamasisha vyuo kuanza kujiandaa na michuano mbalimbali.

Tags: