Maafisa wa serikali wamesema hakuna hatari yoyote kwa wanariadha na mashabiki,ila tu kwa wanawake wajawazito.
Awali, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilikuwa limeonya kuwa virusi vya Zika ni hatari kubwa kwa afya ya umma duniani na kutangaza hali ya tahadhari,huku Shirika hilo likiomba mataifa kuungana kuukabili ugonjwa huo.
Virusi hivyo vimehusishwa na kuzaliwa kwa watoto wanaozaliwa wakiwa na vichwa vidogo na ubongo uliodumaa.
Wataalamu wameonya kwamba virusi hivyo vinavyoenezwa na mbu vinasambaa sana Amerika Kusini na kusababisha madhara makubwa.

