Tuesday , 18th Nov , 2014

Vilabu shiriki vya Ligi kuu tanzania Bara vimetakiwa kufanya usajili kwa kuzingatia mapungufu yaliyopo katika timu.

Akizungumza na East Africa Radio,Kocha Boniface Mkwasa amesema nafasi ya usajili ni sehemu ya kuangalia timu imekosea sehemu gani ndipo wafanye usajili hivyo watakapokosea wataanza kumlaumu kocha ambaye sio mara zote anaweza kuhusika katika suala zima la usajili.

Mkwasa amesema vilabu visitegemee mashabiki wala baadhi ya viongozi kwa ajili ya kufanya usajili suala ambalo hapo baadae linaweza kuwaletea matatizo katika timu.