Akizungumza na East Africa Radio, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Celestine amesema, anayefanya kazi ni lazima alipe kodi na kodi ya mfanyakazi inatokana na mshahara wake kwa maana mchezaji anapopata mshahara mkubwa ndipo kodi inapokatwa kubwa kwani ni wajibu kwa vilabu kufanya hivyo.
Mwesigwa amesema, watafanya utaratibu wa kuwasiliana na TRA ili kutoa elimu kwa vilabu kwani vilabu vyote vinatakiwa kuhakikisha wachezaji wa ndani wamelipia hata wale wa kimataifa pamoja na makocha ambao pia wanalipia vibali vya kazi ambapo makato kwa upande wao yanakuwa tofauti .
Mwesigwa amesema, ulipaji wa kodi utasaidia kuepusha suala la wachezaji kusajiliwa na kulipwa fedha za usajili usiku ambao unakuwa hauna uhakika baina ya mchezaji na muajiri na pia vilabu vyote.
Mwesigwa amesema, pamoja na hayo pia vilabu vitatakiwa kuwa na leseni itakayowezesha kushiriki ligi msimu ujao na kama itakuwa haijatimiza suala la leseni haitaruhusiwa kushiriki ligi hiyo.
